
Mwanachama atoa pongezi kwa Huduma bora za watendaji
Iliyo chapishwa: 15 Oct, 2024
Katika jitihada za kuthamini na kuhamasisha juhudi za wafanyakazi, Hazina SACCOS katika mkutano mkuu wake wa mwaka 2024 imepewa zawadi na mwanachama wake katika kutambua mchango wa chama katika kuleta maendeleo yake na familia yake kiujumla.