1. Utangulizi
Akiba ni fedha anazochangia mwanachama ili kuwa na sifa ya kupata huduma za mikopo. Fedha hii hairuhusiwi kutoka ama kupungua mara kwa mara isipokuwa kama ilivyoelekezwa katika Masharti ya Chama
2. Aina Za Akiba
Hazina Saccos Limited SACCOS Ltd itakuwa na makundi makuu 2 ya Akiba
(a) Akiba Za Lazima
(b) Akiba Za Hiyari
(b) Akiba Za Hiyari
Akiba ya lazima inamfanya mwanachama kuwa na sifa ya kupata huduma ya mikopo na akiba hii haitachezacheza kwa maana ya kutoka ama kupungua kama inavyoelekezwa kwenye Masharti ya Chama
Akiba ya hiyari ni akiba anayojiwekea mwanachama kwa malengo mahsusi na akiba hii inaweza kutolewa ama kupunguzwa muda wowote. Endapo kiwango kinachotolewa ama kupunguzwa ni kikubwa kuliko kiwango kilichowekwa katika Masharti basi Mwanachama atatakiwa kutoa notisi ya siku 14.
3. Aina ya Mazao ya Akiba ya Hiyari
Mwanachama anaweza kuweka akiba yake ya hiyari katika moja ya mazao yafuatayo:-
3. Aina ya Mazao ya Akiba ya Hiyari
Mwanachama anaweza kuweka akiba yake ya hiyari katika moja ya mazao yafuatayo:-
-Akiba Ya Malengo Maalum
(a) Akiba Ya Watoto
(b) Akiba Ya Elimu
(c) Akiba Ya Sikukuu
(d) Akiba Ya Wasitaafu
(e) Akiba Ya Jamii
(f) Akiba Ya Mshahara
(a) Akiba Ya Watoto
(b) Akiba Ya Elimu
(c) Akiba Ya Sikukuu
(d) Akiba Ya Wasitaafu
(e) Akiba Ya Jamii
(f) Akiba Ya Mshahara
4. Riba Juu Ya Akiba
Kila mwaka Hazina Saccos Limited kupitia Mkutano Mkuu itaweka kiwango cha riba juu ya akiba za wanachama ili kuwezesha ongezeko la thamanai ya akiba hizo. Kwakuwa hii ni gharama ya kifedha kwenye Chama itakuwa inabadilika kila mwaka kutokana na mwelekeo wa makisio ya mapato na matumizi.
Mwanachama akikoma kuwa mwanachama wa Hazina SACCOS Ltd atatakiwa kuandika notisi na akiba zake atarejeshewa baada ya siku 90 tokea kupokelewa na notisi hiyo.