Hazina SACCOS inaongozwa na Wajumbe wa Bodi saba na Kamati ya Usimamizi yenye Wajumbe watatu ambao wote ni Watumishi wa Wizara ya fedha na mipango .Pamoja na hao, usimamizi wa shughuli za kila siku za Chama uko chini ya Mtendaji Mkuu na Menejiment yake kwa ujumla. Hazina SACCOS iko chini ya ulezi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Aidha , Chama kinaendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria ya huduma ndogo za fedha na 10 ya mwaka 2018 na sheria ya ushirika namba 6 ya mwaka 2013 pamoja na Masharti ya Chama na sera mbalimbali za Chama.
