Mikopo Yetu
Chagua mkopo unaokufaa na ujue masharti yake kwa urahisi.
1. Mkopo wa Tuliza Moyo
Kiwango cha mkopo huu ni kuanzia Tsh 300,000/= hadi Tsh.1,000,000 bila riba. Muda wa marejesho ni siku 30, mkopo huu hutolewa ndani ya masaa 24 baada ya kukamilisha taratiu za maombi.
2. Mkopo wa Dharura 1
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 5,000,000/= na kutoza riba 1.5% kwa mwezi. Muda wa juu wa marejesho ni miezi 12, mkopo huu hutolewa ndani ya masaa 24 baada ya kukamilisha taratibu za maombi.
3. Mkopo wa Dharura 2
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 10,000,000/= na kutoza riba 1.5% kwa mwezi. Muda wa juu wa marejesho ni miezi 24, mkopo huu hutolewa ndani ya siku saba (07) baada ya kukamilisha taratibu za maombi.
4. Mkopo wa Elimu
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 5,000,000/= na kutoza riba ya 0.42%. Muda wa kurejesha mkopo ni miezi 24. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1 – 20 ya kila mwezi.
5. Mkopo wa Biashara
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84% kwa mwezi. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.
6. Mkopo wa Viwanja
Hutegemea na taratibu zitakazowekwa na chama kwa wakati huo.
7. Mkopo wa Mazishi
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni 3,000,000/= na kutoza riba ya 0.42% . Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 24 , mkopo huu hutolewa pale mwanachama anapokuwa amefiwa baba,mama, mtoto, mume au mke.
8. Mkopo wa sikukuuu
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni 500,000/= na kutoza riba ya 0.84%. Muda wa juu wa kurejesha mkopo ni miezi 6. Hutolewa kwa sikukuu za Krismas, Pasaka, na Idd El-fitri
9. Mkopo wa Maendeleo
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84%. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Hutolewa mwishoni mwa mwezi na fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.
10. Mkopo wa Ujenzi
Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mara tatu (3) ya akiba za mwanachama na kutoza riba ya 0.84% kwa mwezi. Muda wa kurejesha mkopo huu ni miezi 12 – 60. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.
11. Mkopo wa utaratibu wa Bank (Standing Order)
Kiwango cha juu ni Tsh 50,000,000.00 na kutoza riba ya 1.5%. Muda wa kurejesha ni miezi 48. Fomu hupokelewa kuanzia tarehe 1-20 ya kila mwezi.
12. Mkopo wa Ajira Mpya
Ni mkopo kwa ajili ya waaajiriwa wapya wenye ajira isiyozidi miezi 6.Kima cha juu ni Tzs 5,000,000 na atakatwa kiingilio 100,000,hisa 500,000,akiba za miezi mitatu za 300,000, na mkono wa pole Tzs 32,400.
13. Mkopo wa Fastanatoboa
Kiasi cha mkopo huu ni kuanzia Tzs 500,000-5,000,000 na muda wa marejesho ni ndani ya miezi mitano. Riba yake ni 7% kwa miezi mitano.Mkopo huu unatolewa ndani ya masaa 12 ya kazi na baada ya nyaraka kukamilika na kuwasilishwa ofisini.