Maswali Ya Mara Kwa Mara
Je mkopo mkubwa unaenda mpaka kiasi gani?
Mkopo wetu mkubwa ni mpaka TZS 100,000,000/=na unaweza kurejesha ndani ya miezi 60.
Je Nawezaje kujiunga na Hazina SACCOS?
i.Kwa kujaza fomu ya kujiunga inayopatikana kwenye tovuti au ofisini ii.Kulipa ada ya kiingilio TZS 100,000/= iii.Kununua hisa 25@20,000/=
Je nikisahau password ya portal nafanyaje?
Ukisahau password utaandika username yako alafu utachagua option ya forget password ndipo utapokea password mpya kwenye email yako hapohapo
Najiungaje na portal ya Hazina SACCOS?
Kwa mara ya kwanza inabidi utume majina yako matatu,barua pepe na cheki namba kwa afisa ndipo akutengenezee akaunti na kukupa taarifa za kuingilia.
Kwa nini nijiunge Hazina SACCOS?
Kwa sababu ni chama kinachokusaidia kutimiza malengo yako ya kifedha kwa kutoa huduma bora,kwa wakati na riba nafuu.
Je mtu yoyote anaweza kuwa mwanachama wa Hazina SACCOS LTD?
Hapana,ila ni mtu yoyote ambaye ni mtumishi wa umma Tanzania