
Hazina SACCOS Ltd ni chama cha akiba na mikopo chenye usajili namba DSR 1822 kilichoanzishwa mwaka 1972 na kusajiliwa mwaka rasmi Mach 1973 kikiwa na Wanachama 250 waliokuwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Chama kiliendelea kujulikana na kuwa mvuto kwa watumishi wa Wizara na mashirika mbalimbali ya Umma Tanzania bara. Kutokana na watumishi wa Wizara ya fedha kuwa walikuwa wanahamishwa kwenda sehemu zingine nje ya Wizara ya fedha, taarifa za Hazina SACCOS zilisambaa nchi nzima na kusababisha watumishi hao kuwa wanakuja kuomba uanachama Hazina SACCOS. Mnamo Mwaka 2010, Chama kilifungua fungamanisho kutoka kuhudumia watumishi wa Wizara ya Fedha kuanza kuhudumia Watumishi wa Umma Tanzania bara. Aidha, mnamo Julai 2022, chama kilifunga tena fungamanisho kutoka kuhudumia Watumishi wa Umma Tanzania bara kwenda Watumishi wa Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Hazina SACCOS Ltd inatoa huduma za kukopesha na kukusanya akiba na hisa miongoni mwa Wanachama wake. Hazina SACCOS Ltd ina aina tisa za mikopo inayotolewa kwa wanachama wake, ambazo ni Maendeleo, Biashara, Viwanja, Maalum, Ujenzi, Elimu, Dharura, Sikukuu, na Mazishi. Aidha, Hazina SACCOS Ltd ina aina mbalimbali za mazao ya akiba, ikiwa ni Akiba ya Lazima na Amana. Sambamba na hiyo, pia inapokea hisa za aina mbili ambazo ni Hisa za Lazima na Hisa za Hiari. Hazina SACCOS Ltd imeweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa ni kuongeza hisa na kukuza akiba za wanachama, kuongeza idadi ya wanachama, kuongeza mtaji na idadi ya wanachama. Pamoja na mambo mengine, Hazina SACCOS Ltd imefanikiwa katika kuboresha maisha ya Wanachama wake kwa kuanzisha eneo la Ihumwa Ngaloni na Iyumbu East kwa ajili ya makazi ya Wanachama wake.